[…itakuwa ni Franklin Bulls wanaotangulia kupata umiliki na moja kwa moja Payton Hughes anaupata mpira na kujaribu kuupiga lakini Kendry Rams wanaiba mpira mapema ili kutafuta shambulizi la haraka. Hapo yupo kijana Tom Isaac. Tom Isaac hakujihusisha kwenye safu ya ulinzi ya mchezo huo. Anaotea tu. Hajihusishi na ulinzi kabisa. Wapo kwenye ulinzi wa eneo, yaani eneo la sanduku, kisha wanamuacha nje tu. Wanajaribu kupiga pasi ndefu ya aina ya “Salamu Maria”, lakini Bulls wanarudi kwa haraka. Hakuna nafasi kwa “Salamu Maria” hiyo. Mbinu ya kuvutia sana! Naam, ni mtazamo wa kufurahisha sana- katika muda wote wa ulinzi Isaac amekuwa katika upande huu wa kiwanja. Sasa anajaribu mpira wa pointi tatu, akitaka tena kufunga mfululizo lakini hapati. Je, wanaweza kupata fursa ya mashambulizi pia? Martin! Hiyo ilikuwa nafasi nzuri ya pili kwa upande wa Rams. Tena, hajihusishi katika mchezo. Sijawahi kuona jambo kama hili kwenye mchezo wa kikapu. Ni jambo la kufurahisha kutoka upande wa Rams- jambo la ajabu sana…]